Maisha mapya katika Yesu Kristo huleta mabadiliko haya…
1 Haja ya kutaka kulijua Neno la Mungu katika Biblia. “Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ila kwa hayo mpate kuukulia wokovu…” 1 Petro 2:2
2 Haja ya kumtii Yesu Kristo. “Mkinipenda mtazishika amri zangu” Yohana 14:15
3 Kusikitishwa na dhambi. Hatuwezi kufurahia dhambi tena. “…Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.” 2 Timotheo 2:19
4 Kuwatafuta waliopotea. Wale ambao bado hawaja tubu na bado hawajamfahamu Mungu kibinafsi. “…bali huvumumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikilie toba.” 2 Petro 3:9 |