Sababu nne za kukujulisha kuwa umeokolewa:
1 Umetii amri za Mungu kwa kutubu na kuamini, na ni Mwaminifu katika kutunza Maneno yake. “Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele.” 1 Yohana 5:13
2 Una ujasiri katika damu ya Kristo iliyomwagika msalabani. “Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.” Waefeso 1:7
3 Umeacha kujitegemea mwenyewe katika kuendesha maisha yako na badala yake
umempatia Yesu Kristo, Bwana aliyefufuka, mwenye haki zote. “Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu,Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye” Wakolosai 2:6
4 Tayari Mungu ameweka Roho wake Mtakatifu ndani yako.Katika roho yako mwenyewe anakuhakikishia kuwa u wake. “Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu” Warumi 8:16 |