Imani Iokoayo Katika Bwana Yesu
Umejiandaa kujitoa kikamilifu kwa jinsi ulivyo na vyote ulivyo navyo kwa ajili ya utawala wa Bwana Yesu Kristo.
Ni mabadiliko ya utawala katika moyo wako kutoka katika kujitawla mwenyewe na sasa kuwa chini ya utawala wa Bwana Yesu Kristo. Kwakuwa Kristo ni Mungu na alikufa na kufufuka kutoka kwa wafu kwa ajili yako, Yeye ni muhimu kuliko kazi yako, familia,fedha, ajira, na hata maisha yako yenyewe. Mathayo 10:37-39, Luka 9:57-62, 1 Wakorinto 15:3,4.
Katika Luka 14:26, Yesu anasema kwamba mtu akitaka kuwa mfuasi wake, lazima amtangulize Yeye kwanza kabla ya baba na mama yake, mke na watoto, nduguze. Naam, na hata maisha yake mwenyewe, ama sivyo hawezi kuwa mfuasi wake.
Unapojitoa kwakwe na kumuamini Yeye kabisa, Mungu ataweka Roho yake ndani yako na utazaliwa katika familia yake. Mungu sasa anakuwa baba mwenye upendo na anaweza kufanya mabadiliko katika maisha yako kadiri atakavyo - popote na wakati wowote.
“Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka…” Matendo 16:31 |