<<<<<

Piga
Mungu
Pengine
Huyu
Kila
Kutojali
Kujali
Amri Kumi
Hatia
Umepata
Toba
Basi
Imani iokoayo
Anakuwa
Kwa
Sababu
Na

Barua-pepe

  >>>>>

Toba


Una mabadiliko makubwa ya mawazo na moyo na unachagua kuzikataa na kuziacha dhambi zote zifahamikazo na haki ya kujiendeshea maisha yako wewe mwenyewe bila kumtegemea Mungu.

Toba Ni tendo la kujivua fahari ya maisha yako ya kujitegemea mwenyewe na kumkabidhi Yesu Kristo aweze kuchukua nafasi yake halisi.

Toba Ni kugeuka kabisa kiroho na ni lazima kabla ya kuamini.

Toba Si suala la kuwa tu na huzuni kwa ajili ya dhambi zako. Katika toba kuna huzuni, lakini unaweza kuwa na huzuni bila hata ya kutubu. Watu wengi hujutia matokeo ya dhambi zao, lakini hawajuti juu ya dhambi yenyewe. “Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.” 2 Wakorintho 7:10

Toba Si jambo tu la kuacha matendo ya dhambi. Baadhi ya watu hujinasua kutoka katika dhambi fulani kutokana na sababu binafsi (afya, heshima, familia, biashara, nk.), si kwa sababu dhambi zao zilimchukiza Mungu.