Pengine tayari unafahamu jambo fulani kuhusu Mungu, lakini hapa kuna mambo makuu muhimu matatu ambayo unapaswa kuyazingatia.
…Yeye ni mwenye hekima na anafahamu kipi ni muhimu kwa maisha yako.
…Yeye ni mtakatifu, hawezi kukubali dhambi na atatoa hukumu.
…Yeye mwenye rehema hivyo Anaweza kubadilisha hukumu na kukusamehe kwa kifo cha Yesu
msalabani. “Ni nani Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu…” Mika 7:18
Yesu Kristo ndiye njia pekee ya kwenda kwa Mungu, kwa kuwa anasema “…Mimi ndimi njia,na kweli,
na uzima;mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Yohana 14:6
Je, umewahi kujiuliza…
Je, lengo kuu la maisha ni lipi?
Wengine husema - kufurahi na familia yangu, kuwa mwenye furaha, kuishi maisha mema, kuridhika. Haya ni mazuri, lakini Biblia inatuambia lengo kuu ni hasa kumfahamu Mungu kwa uzoefu upatikanao kwa Yesu Kristo. Fikiri juu ya hilo! Hakika unaweza kumfahamu Mungu kama unavyoweza kumfahamu rafiki yako.
“Na uzima wa milele ndio huu,Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli,na Yesu Kristo uliyemtuma.” Yohana 17:3 |